MSD Yapongezwa Ujenzi Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitihada kubwa inazozizifanya kuboreshaji upatikanaji wa bidhaa za afya nchini kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na kuboresha viwanda vya dawa vilivyokuwa na hali mbaya.
Sillo ametoa pongezi hizo leo, Kamati hiyo ilipokuwa ziarani MSD, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa Kamati hiyo walitembelea kiwanda cha dawa cha Keko, kiwanda cha MSD cha kuzalisha Barakoa pamoja na Maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya dawa yaliyopo keko.
Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Barakoa cha MSD, Bw. Twahil Magoolo akitoa maelezo juu ya uzalishaji Barakoa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Wakati Kamati hiyo Ilipotembelea kiwandani hapo
Amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze na watendaji wote wa MSD kwa maono yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba kwani ununuzi bidhaa hizo kutoka nje ya nchi na kwingineko umekuwa ukiigharimu serikali fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha huduma nyingine.
mbele, tunazichukua na kuzifikisha serikalini ili kuhakikisha MSD inaimarika ipasavyo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa nchini".
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Wakipokea Maelezo kuhusu dawa, kutoka kwa Msimamizi ya Kiwanda cha Dawa cha Keko, Bi. Bettia Kaema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze katika taarifa yake ya utendaji aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD bado inaendelea kutoa huduma bora na za kiwango cha juu kwa wananchi na kusimamia mnyororo wa ugavi, ili kuleta tija kwenye mfumo wa afya wa nchi. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Wakati Kamati hiyo Ilipotembelea Makao Makuu ya MSD, jijini Dar es Salaam |
N