MSD Yaahidi Kuendeleza Ushirikiano na Wadau
Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa MSD Bw. Christopher Kamugisha akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Mashirikiano na Wadau Watendaji wa Mnyroro Ugavi, Jijini Dar es Salaam.
Bohari ya Dawa (MSD) imeahidi kuendelea kushirikiana na washirika na wadu mbalimbali ili kuendelea kuboresha na kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, kwenye Mkutano wa Mashirikiano na Wadau Watendaji wa Mnyroro Ugavi, ulifanyika katika Ukimbi wa New Africa Hotel jijini Dar es salaam; Mshauri wa Masuala ya Kisheria wa MSD Bw. Christopher Kamugisha, amesema MSD imeendelea kujiimarisha kiutendaji katika nyanja mbalimbali za Mnyororo wa ugavi, kuanzia ununuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa za afya ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo nchini. Wadau Mbalimbali Wakisikiliza Mada, Wakati wa Mkutano wa Mashirikiano na Wadau Watendaji wa Mnyroro Ugavi
Bw. Kamugisha amesisitiza kwamba MSD inaendelea kupokea ushauri na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau ili kwa pamoja kuweza kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.
Aidha, ameongeza kwamba bado mnyororo wa ugavi nchini unakabiliwa nao changamoto japo kwa uchache, hivyo ni jukumu la wadau kupitia kikao hicho kuweza kuzijadili na kuzitaftia tatuzi ilikuboresha afya za wananchi. Wadau wa Mnyroro wa Ugavi wa Bidhaa za Afya Wakisikiliza Mada
|
N