MSD Yaendesha Mafunzo ya Tehama kwa Watumishi Wake

1111111.jpg

                           Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala MSD Bw. Erick Mapunda,

                                               Akisisitiza Jambo Wakati wa Mafunzo

 

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD Bw. Erick Mapunda amewaasa watumishi wa MSD kutotumia vibaya mifumo ya taasisi kwa kufanya matendo yasiyofuata utaratibu na kanuni za utumishi wa umma, bali watumie uzoefu wao kubaini changamoto zote za kimfumo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na kuhakikisha Taasisi inafikia malengo yake.

 

Bw. Mapunda ametoa rai hiyo hii leo tarehe 9/8/2021 jijini Dar es salaam, wakati akifungua mafunzo ya siku 7 yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa MSD juu ya maboresho ya Mfumo wake wa EPICOR 10, uliohuishwa hivi karibuni ili kuboresha huduma kwa wateja.

 

Bw. Mapunda amewasihi watumishi hao kutoka Ofisi za Kanda, Makao Makuu na Maduka ya MSD kuongeza juhudi katika kujifunza mambo mapya yaliyoboreshwa kwenye mfumo, ili kuboresha huduma kwa mteja.

 

“Tumieni fursa hii kujifunza mambo mapya yaliyohuishwa kwenye mfumo, najua mmekua mkitumia mfumo huu kwenye kazi zenu za kila siku, hakikisheni hamtumii changamoto za mfumo huu katika matendo yasiyofuta kanuni na taratibu. “Alisema Bw. Mapunda

 


44444.jpg
            
                                          Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA MSD Bi. Habiba Issa,

                                           Akitoa Mada Wakati wa Mafunzo ya TEHAMA

Naye Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Bi. Habiba Issa amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa MSD kwa kukubali mafunzo hayo yafanyike, kwani yatasaidia kuwajengea uwezo watumishi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoboreshwa

 

“Kuna vitu vingi vipya vimeogezwa kwenye mfumo ambavyo watumiaji wanatakiwa wafundishwe ili kuboresha utendaji wao na huduma kwa wateja wetu” Alisema Bi. Habiba.


77777777.jpg

                                 Watumishi wa MSD Wakifuatilia Mada Wakati wa Mafunzo ya TEHAMA

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker