Wataalamu Kutoka Muhimbili Watembelea MSD
Baadhi ya madaktari na Wataalam wa baabara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Mloganzila wametambulishwa mashine na vitendanishi vya maabara vipya vinavyonunuliwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa matumizi ya vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali nchini.
Mtaalam wa maabara wa MSD Joseph Kitukulu amewaeleza kuwa,mbali na vifaa hivyo kutumia teknolojia ya kisasa, kupunguza muda na kuwa na gharama nafuu vinauwezo wa kuchukua sampuli nyingi zaidi.
Kwa upande wake,Msimamizi wa Utekeleza Mpango Mkakati wa MSD, Bi. Neema Mwale amesema kuwa hatua ya MSD kununua vifaa hivyo kutoka kwa wazalishaji itachangia juhudi za serikali kuboresha huduma za afya za wananchi na kuipunguzia serikali gharama kwa takribani asilimia 40 hadi 50.
|