Matumizi ya Cheti cha Dawa Kilichoboreshwa

MSASI_PRESS.png

                                                   Mfamasia Mkuu wa Serikali, Bw. Daudi Msasi

Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi, amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa, Halmashauri, Waganga Wafawidhi na Wafamasia kote nchini Kuzingatia na kusimamia matumizi ya miongozo na nyenzo za usimamizi wa bidhaa za afya, ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa dawa vituoni.

 Bw. Msasi amesisitiza kwamba kutozingatia matumizi sahihi ya miongozo na nyenzo muhimu katika utunzaji na utoaji wa dawa, kumekuwa kukisababisha changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

 Bw. Msasi ametoa rai hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kufafanua kuhusu matumizi ya cheti cha dawa kwa ngazi zote za kutolea huduma za afya nchini.

 Aidha, Bw. Msasi amevielekeza vituo vya kutolea huduma za afya nchini kuhakikisha vinanunua vitabu vya “Prescription” ya dawa vilivyoboreshwa kutoka MSD, na pale vinapokosena kwenye Bohari basi wapakue kutoka tovuti ya Wizara ya afya.

 

IMG_20210703_113328_284.jpg

                             Bw. Daudi Msasi akizungumza mbele ya waandishi wa habari

Ameongeza kuwa vitabu hivyo vya “Prescription” iliyoboreshwa vitaanza rasmi kutumika kuanzia julai 10, mwaka 2021, lengo likiwa ni kuwezesha kutunza kumbukumbu sahihi za matumizi ya dawa na kurahisisha ufuatiliaje wake.

Tayari Bohari ya Dawa (MSD), imekwisha chapisha jumla ya Vitabu vya “ Prescription” takribani elfu sitini na tano (65,000), vikingoja kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker