Mawaziri wa Afya wa SADC Waitembelea MSD

4.jpg

                                 (Mawaziri wa Afya kutoka nchi za SADC wakimakinikia mada, mara walipotembelea MSD)

               Mawaziri kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa

                (SADC) wanaoshughulikia masuala ya Afya na Ukimwi

           wametembelea Ofisi za Bohari ya Dawa (MSD) zilizoko Keko,

                  jijini Dar es Salaam nakushuhudia jinsi mnyororo

                            mzima wa ugavi unavyofanya kazi.

 

                 Mawaziri hao wameonyesha kuridhishwa na kufurahishwa

                   na jinsi MSD ilivyojipanga katika kutekeleza majukumu

               yake kwa ufanisi,mathalani ununuzi, uhifadhi, na usambazaji

                     wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara huku

              wakibainishakuwa ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama.

3.jpg

                     (Mawaziri wa Afya kutoka nchi za SADC wakimakinikia mada,

                                mara walipotembelea Bohari ya Dawa (MSD))

        Mawaziri hao wanaoshughulika na afya wameambatana na mwenyeji

             wao Waziri wa afya wa Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb),

               ambaye amewaeleza waandishi wa habari utayari wa MSD

                 katika katika kufanya manunuzi ya pamoja kwa nchi

              za SADC na mchakato mzima uliopelekea MSD kupewa

                                              zabuni hiyo.

 

 

                 Aidha, amebainisha kuwa lengo la ziara hiyo ya Mawaziri

                 ni kuangalia uwezo, vifaa na utaalamu wa MSD katika

                     kutekeleza majukumu hayo kwa nchi wanachama.

 

index2.jpg

                           (Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akitoa mada)

               Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean             

             Bwanakunu, ametoa tathimini ya ulipofikia mchakato mzima

          wa manunuzi ya pamoja, kwa nchi wanachama hadi sasa (SPPS),

             ambapo amebainisha kwamba wamekwisha pata wazabuni

                     na sasa mikataba iko kwa Mwanasheria Mkuu

                                 ikifanyiwa upembuzi, (Vetting).

 

 

               Aidha amewahakikishia mawaziri hao kutoka SADC kuwa

        mchakato wa manunuzi ya pamoja utapunguza gharama kwa kiasi

      kikubwa kwa nchi wanachama na kukuza uchumi wa viwanda kupitia

                                     uwekezaji wa viwanda vya dawa.

 

 

               Mawaziri hao kutoka SADC, walipata fursa ya kutembelea

              magahala ya kuhifadhia dawa ya MSD na kujionea jinsi kazi

               mbalimbali za utunzaji na ugavi, zinavyofanyika kwa weledi

                                         na ufanisi mkubwa.

 

index.jpg

(Meneja Mradi Msonge wa MSD Bw. Bill Singano, akitoa ufafanuzi mbele ya mawaziri wa Afya wa SADC)
 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker