DKT. Shein Amwaga Pongezi kwa MSD.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza MSD kwa kuteuliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa ajili ya nchi za SADC.
Dkt. Shein alimweleza hayo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alipotembelea banda la MSD katika maonesho ya viwanda yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kingozi huyo pia ameishauri MSD kuwatembelea wazalishaji wakubwa wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wa mataifa ili wapate taarifa sahihi na kuwashirikisha kuhusu MSD kuteuliwa kusimamia manunuzi ya pamoja ya dawa kwa nchi za SADC.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya manunuzi ya pamoja, ambapo tayari wameanza mchakato wa kupata wazabuni na kuanzisha mfumo wa kielektroniki utakaotumiwa na nchi wanachama kuleta mahitaji.
Bohari ya Dawa MSD, ni moja ya taasisi zilizoshiriki maonyesho ya biashara na viwanda ya SADC yaliyofanyika wakati wa wiki ya mkutano wa SADC 2019, katika viwanja vya kimataifa vya Julius Nyerere jijini Dar es salaam. |