MSD Yawasilisha Msaada wa Dharura kwa Majeruhi wa Ajali ya Moto Mkoani Morogoro
,
Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto, iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia ulilenga kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.
Aidha, Bohari ya Dawa imechukua jitahada za makusudi kwa kusafirisha shehena hiyo kutoka kwenye magahala yake jijini Dar es salaam, ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu.
|