Waziri Ummy Mwalimu, Ahimiza Ujenzi wa Viwanda vya Dawa Nchini
, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema serikali inawajengea mazingira mazuri wazalishaji dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wanaowekeza nchini kwani wanasaidia kupunguza gharama za kuagiza dawa nje ya nchi.
Waziri Huyo ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Tatu wa mwaka wa wazalishaji na wasambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mkutano huo umeandaliwa na Bohari ya Dawa kwa kushirikiana na UNDP ambapo mwakilishi wa UNDP Dr. Rosemary Kumwenda amesema mkutano huu ni muhimu kwani MSD kwa sasa inafanya kazi kimataifa na UNDP kama wakala wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa inawajibu wa kuunga mkono jitiada za MSD kuhakikisha shughuli zinazofanywa na MSD zinakuwa na manufaa kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema wameandaa mkutano huo ili kuweka mazingira ya uwazi na kuboresha utendaji wa MSD na kuwavutia wazalishaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kuja kuwekeza. |