Waziri Bashungwa Asema Serikali Imeweka Mazingira Rafiki kwa Uanzishwaji wa Viwanda Nchini
,
Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Mhe. Innocent Bashungwa amefungua mkutano wa kwanza wa kimataifa wa wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba,ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD).
Waziri huyo ameeleza kuwa kufuatia sera ya Tanzania ya viwanda, serikali imewekamazingira rafiki ya uwekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa nchini ili kuwawezesha wawekezaji wenye nia.
Amesema hatua hiyo itapunguza pia utegemezi mkubwa wa dawa na vifaa tiba kutokanje ya nchi, kwani kwa sasa taifa linapoteza fedha nyingi za kigeni katika kununulia bidhaa hizo za afya.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema wameandaa mkutano huo ili kuweka mazingira ya uwazi kupata wawekezaji,ambapo wamewaeleza matokeo ya utafiti uliofanywa na mshauri mwelekezi wa mradi wa uanzishaji viwanda vya dawa kwa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi.
|