Waziri Ummy Aipongeza MSD Kununua Dawa SADC
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Mb) amesema hatua ya MSD kununua dawa za SADC itasaidia kupunguza gharama za kununua dawa kwa nchi husika na kuboresha upatikanaji wa dawa.
Ameeleza kuwa kwa nchi moja moja kununua dawa ni gharama, ndio maana serikali ya Tanzania kupitia MSD imeteuliwa kufanya manunuzi ya pamoja ya dawa kwa nchi hizo,na tayari wameshatangaza zabuni.
Waziri huyo ameeleza hayo kwa waandishi alipotembelea banda la MSD kwenye Maonesho ya wiki ya viwanda yanayoendelea jijini Dar es Salaam yanayoshirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Maonesho ya viwanda ni utangulizi wa mkutano wa 39 wa SADC 2019, ambao mwaka huu Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo .
|