MSD na SADC Wajadili Muongozo wa Manunuzi ya Pamoja ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

 

 

 

 

626963FD-CE3A-41E5-B318-3000BD2C6C78.jpeg

Bohari ya Dawa (MSD) kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeratibu Mkutano wa wataalamu wa manunuzi ya pamoja (SADC Pooled Procurement Services (SPPS) unaofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kupitia mwongozo wa manunuzi wa pamoja wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi wanachama wa SADC. 

Akifungua mkutano huo, Mfamasia Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Daudi Msasi amewashukuru wawakilishi wa nchi wanachama wa SADC kwa kuitikia wito wa kushiriki kwenye mkutano huo na kwa kuiamini Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa za pamoja. 

Aidha Bw. Msasi pia ameeleza kuwa MSD imekuwa miongoni mwa taasisi bora barani Afrika zinazo shughulika na mnyororo wa ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara. 


3CDE457D-B3FD-4B16-A9ED-2E12224BDA1C.jpeg

 

 

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD Bw. Abdul Mwanja amesema MSD imejipanga kuanza utekelezaji wa jukumu hilo na tayari imeshatekeleza jukumu hilo kama lilivyoainishwa katika Hati ya Makubaliano na Sekretariati ya SADC (MoU) kwa kuanzisha kitengo kitakachoshughulikia manunuzi hayo kwa upande wa SADC. 

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema, faida ambazo nchi wanachama wa SADC watazipata ni pamoja na kupata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa bei nafuu na vyenye ubora, kuboresha kiwango cha usambazaji kwa kila nchi mwanachama. 


CAB58CBD-363C-4E50-B6D1-BFE8B3E18AA6.jpeg

 

Ameongeza kuwa kupatikana kwa fursa hii ni heshima kubwa kwa Tanzania, hatua ambayo italeta ushirikiano ndani ya kanda na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, pia kuongeza fursa uwekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba kwa nchi za SADC na nje, hivyo kupanua soko.

 

Tanzania kupitia MSD ilishinda zabuni ya kuwa mnunua wa pamoja wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa niaba ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

 

1DF4DD23-E561-4819-A056-047319435CC2.jpeg

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker