Tanzania Yatoa Msaada wa Dawa, Vifaa Tiba na Chakula

2C960A10-A632-46B2-AC3A-495762E3C5D8.jpeg

 

 

 

Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa Dawa na Vifaa Tiba na vyakula kwa nchi tatu za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kufuatia kimbunga cha IDAI kilichotokea hivi karibuni kwenye nchi hizo. Kimbunga hiko kimesababisha maafa ya watu kadhaa huku wengine wakikosa makazi.

 

Wakizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.  Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi a, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wamesema msaada huo ni agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean R. Bwanakunu amesema dawa na vifaa tiba vyote vilivyotolewa havitaathiri upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za Afya nchini,kwani dawa zipo za kutosheleza mahitaji ya nchi.

 

Naye Mkuu wa Mafunzo na Utendaji wa Kivita Kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali Francis Shirima ambao ndio wamepewa kazi ya kusafirisha msaada huo na Serikali amesema kazi hiyo itafanyika leo na kuwafikia walengwa kama ilivyooagizwa.

 

Kwa upande wao mabalozi wanaoziwakilisha nchi hizo hapa nchini, Balozi wa Msumbiji, Bi.Monica Mussa, Glad Chembe Munthali- Balozi wa  Malawi na Martine Tavenyika - wa  Zimbabwe wameshukuru kwa msaada huo na kusema Tanzania imeonyesha dira ya ushirikiano mwema.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker