Mkuu wa JKT Atembelea MSD
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw.Laurean R. Bwanakunu juu ya ushirikiano uliopo kati ya MSD na JKT na namna ya kuboresha ushirikiano huo.
MSD inatumia huduma mbalimbali zinazotolewa na JKT ikiwemo ulinzi kupitia Shirika lake la SUMA JKT na ujenzi wa majengo mbalimbali ya MSD ikiwamo maduka ya dawa ya MSD.
Kwa upande wa MSD inatoa huduma pia kwa JKT zikiwemo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya vituo vya Afya vilivyopo chini ya Jeshi hilo.
Viongozi hao pia wamefanya mazungumzo juu ya ushirikiano wa masuala mengine ya kiutendaji baina ya Taasisi hizi.