Mwenyekiti wa Bodi MSD, Aipongenza Menejimenti ya MSD na Wafanyakazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho ameipongeza Menejimenti ya Bohari ya Dawa(MSD) kwa kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa wateja wake pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri na wadau wake mbalimbali.
Dkt.Mrisho amesema hayo alipokuwa akifungua kikao cha 17 cha Baraza la wafanyakazi la MSD,kinachoendelea mjini Dodoma.
Mwenyekiti huyo amewataka watumishi wa MSD kuhakikisha wanafanya kazi kwa umakini kwa kuzingatia dhamira na nia ya kuundwa kwa MSD inafanikiwa,kwa kuhakikisha dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vyenye ubora vinapatikana nchi nzima na kwa nchi za Ukanda wa SADC kwa wakati na kwa bei nafuu.