Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdulla ametembelea Bohari ya Dawa(MSD)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdulla ametembelea Bohari ya Dawa(MSD),ambapo ameishukuru MSD kwa kuwapatia huduma ya dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara visiwani humo na kuwajengea uwezo katika mnyororo wa ugavi wa dawa.

Katibu Mkuu huyo amesema tangu waingie makubaliano ya ushirikiano na MSD ya kuwasambazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, hali ya upatikanaji wa dawa visiwani humo imeimarika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema watahakikisha wanakidhi kila hitaji kutoka visiwani Zanzibar.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker