Bohari ya Dawa (MSD), imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara

Bohari ya Dawa (MSD), leo imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara jijini Dar es salaam, wenye lengo la kujadili kwa pamoja juu ya changamoto, maboresho, taratibu na sheria mbalimbali za manunuzi zinazotumika hapa nchini, sambamba na kuwashawishi wazalishaji hao kuja kuwekeza nchini kupitia viwanda vya dawa.Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema MSD imejiimarisha na kujijengea uwezo wa kuwahudumia wateja wake, hivyo inapaswa kuwa na uhakika na upatikanaji wa dawa zenye viwango na ubora unaokubalika.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole Gabriel amewahamasisha wazalishaji hao kuchangamkia fursa adhimu ya kuanzisha viwanda vya dawa hapa nchini, kwa kuwa mahitaji ya viwanda vya dawa ni makubwa na kuongeza kuwa, uwepo wa viwanda hivyo utarahisisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema mkutano huo ni hatua muhimu ya kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa pande zote mbili wakati wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha na kurahisisha mazingira ya kibiashara. Mkutano huo ulioenda pamoja na majadiliano umefanyika ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara kati ya wadau hao na MSD, ili kuleta tija katika uzalishaji na upatikanaji wa dawa nchini.

Jumla ya wazalishaji 130 kutoka zaidi ya nchi 25 wameshiriki mkutano huo ikiwa ni pamoja na wadau wengine wa MSD.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker