Naibu Waziri wa Afya atembelea MSD

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile leo ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pamoja na mambo mengine amepata taarifa ya utendaji ya MSD kuhusu usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kusema kuwa bajeti ya dawa inayotolewa na serikali iendane na hali halisi ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.

Naibu waziri huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea MSD tangu ateuliwe kwenye nafasi hiyo, amesema hatua ya serikali kuongeza bajeti ya dawa kuanzia mwaka wa fedha uliopita na mwaka huu ina lengo la kupunguza gharama ya dawa na kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vituo vyote vya Afya vya umma ili kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu.

Kwa upande mwingine Mhe. Ndugulile amewataka watendaji wa MSD kuwa na utaratibu wa kuwatembelea wateja wao ili kuboresha huduma zaidi baada ya kusikiliza maoni, malalamiko n a hata ushauri wao. Sambambana hilo amewaagiza  MSD kitengo cha huduma kwa wateja kutembelea wateja wao na kuhakikisha kitengo cha Manununuzi Maalumu (Special Procurement) kinaongeza kasi kwenye manunuzi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa kutokana na hatua ya MSD kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, bei ya dawa na vifaa tiba imekuwa nafuu kwa watumiaji na kueleza kuwa mpaka sasa tayari MSD imetoa mikataba kwa wazalishaji 104, ambapo 11 kati yao ni kutoka ndani ya nchi. Mikataba hiyo ni kwa ajili ya dawa na vifaa tiba takribani  700.

Aidha, ameeleza kuwa kiutaratibu MSD hupeleka dawa moja kwa moja vituoni mara nne kwa mwaka, yaani kila baada ya miezi mitatu, mpango wa MSD sasa hivi ni kufikisha dawa hizo kila baada ya miezi miwili kwa mwaka mzima. Amesema hatua hiyo ya kupeleka dawa moja kwa moja vituoni itapelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nyakati zote vituoni, hasa maeneo ya vijijini.

Naibu Waziri huyo ameipongeza MSD kwa koboresha utendaji wake, hasa katika hatua ya kupunguza muda wa taratibu za ununuzi kutoka miezi tisa hadi miezi sita kwa ajili ya kukamilisha mchakato mzima wa manunuzi, kwa kufuata sheria na taratibu za ununuzi wa Umma. Kaatika ziara hiyo, Mhe. Ndugulile amepewa taarifa ya kitengo cha ufuatiliaji wa mwenendo wa kazi za kila siku za MSD, kijulikancho kama Strategic management office (SMO) ambacho kiko chini ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu. Amewapogenza watendaji wote wa MSD kwa mabadiliko wanayofanya hasa kwa wateja wao na watanzania kwa ujumla.

Naibu Waziri huyo amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) tangu mwezi Septemba, 2012 hadi mwezi Julai, 2016.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker