MSD kusambaza dawa kwa kutumia Drones

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa (MSD) wamesaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Zipline International Inc. kwa ajili ya huduma ya kusafirisha dawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones) kwenye maeneo magumu kufikika. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya huduma hii itaanza kutumika kuanzia mwaka 2018,kwa kuanza na majaribio kwenye Kanda za MSD za Dodoma na Mwanza ambapo jumla ya mikoa 10 itafaidika na baadae kupanua huduma hiyo kwa nchi nzima ili kuhakikisha dawa muhimu zinawafikia wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD,Bw.Laurean Bwanakunu amesema dawa muhimu zitakazosafirishwa na ndege hizo zisizo na rubani ni pamoja na chanjo, dawa za kuokoa maisha kama dawa ya kuongeza damu (Folic&Ferus),dawa ya kuzuia kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua (Oxtocin) na dawa za kutibu Pneumonia kwa watoto (Amoxicillin DT) na dawa ya kuzuia kifafa cha mimba (Magnesium Sulphate Injection). Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zipline Keller Rinaudo amesema kuwa watakuwa na vituo vinne vya kurushia ndege hizo zisizo na rubani ambacho kila kimoja kitakuwa na ndege 30 ambazo zitakuwa na uwezo wa safari 500 kwa siku.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker