Bohari ya Dawa (MSD) yapokea msaada wa shilingi Mil. 25

Bohari ya Dawa (MSD) imepokea msaada wa shilingi Mil. 25kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya kuendeleza mpango wa kuendesha maduka ya dawa ya MSD.

Akizungumza wakati wa shughuli ya makabidhiano ya hundi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuanzisha Duka la dawa Mkoani Rukwa ambapo tayari amefanya mazungumzo na uongozi wa Mkoa huo kuandaa taratibu za kusogeza huduma ya dawa kwa wananchi.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa NMB Bw. Richard Makungwa ameeleza kuwa Sekta ya Afya ni moja ya maeneo wanayoyapa kipaumbele katika huduma za jamii. Awali NMB walishaipatia MSD Mil.5 ambapo pamoja na msaada wa leo inakuwa Mil.30 kwa ajili ya Duka la dawa la Mkoa wa Rukwa.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker