MSD yakutana na washitiri na wazalishaji

Bohari ya dawa (MSD) imefanya mkutano na washitiri, watoa huduma na wazalishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wanaotoka ndani na nje ya nchi kujadili kuhusu maboresho ya manunuzi ya bidhaa za MSD.

Takribani wazalishaji hao wanatoka nchi za Kenya, Uganda, India, Bangladesh, China, Korea, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika Kusini.

Mkutano huo pia umehusisha wadau wakuu wa MSD kutoka Baraza la Famasi Tanzania, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema mkutano huu hufanyika kila mwaka lakini mwaka huu watajikita Zaidi kujadili namna MSD ilivyoboresha mfumo wake wa utendaji hasa hatua ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji pamoja na kuboresha taratibu za manunuzi ikiwa ni pamoja na kupunguza mlolongo mrefu wa taratibu za manunuzi.
Hadi sasa tayari MSD ina mikataba 73 ya wazalishaji wa dawa na vifaa tiba, ambapo kati ya hao tisa ni wazalishaji wa ndani.
Wazalishaji hao walipata pia fursa ya kuuliza maswali, kutoa ushauri na kujadiliana namna ya kuboresha uhusiano wa kubiashara na MSD kwa faida ya Jamii ya Tanzania inayohudumiwa na MSD.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker