MSD yakarabati Ghala la dawa la Mirembe


Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na ukarabati huo,watoa ushieikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa yenye utaalamu unaohitajika.Ameongeza kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo,ikiwa ni pamoja na kukopeshwa,kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na kuomba ushirikiano zaidi na MSD,ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker