WAWEKEZAJI KUTOKA MISRI WATEMBELEA ENEO LA MSD KIBAHA
Baada ya Bohari ya dawa (MSD) kusaini makubaliano ya kumiliki eneo la ardhi lililopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha,kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya kuzalisha dawa kwa ubia na sekta binafsi,baadhi ya wawekezaji wameanza kufika kuangalia mazingira ya eneo hilo.
Wawekezaji hao kutoka nchini Misri walifika kuonyeshwa eneo hilo na kufanya majadiliano na Mkurugenzi Mkuu Bwana Laurean Bwanakunu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi. Victoria Elangwa na Meneja Miradi Bwana Fredrick Pondamali pamoja na watu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bwana Clifford Tandari na Wizara ya Afya.
Kufika kwa wawekezaji hao kuangalia eneo la kuwekeza ni matokeo ya mkutano kati ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Johm Pombe Magufuli na Raisi wa Misri Mheshimiwa General Abdel Fattah el-Sisi walipofanya mazungumzo wakati wa mkutano wa umoja wa Afrika uliofanyika mapema mwaka huu.