Mchakato wa kuanzisha viwanda vya kuzalishia dawa na vifaa tiba
Bohari ya Dawa(MSD) ipo kwenye mchakato wa kuanzisha viwanda vya kuzalishia dawa na vifaa tiba nchini kupitia mpango wa public–private partnership (PPP). Leo hii timu ya MSD imekwenda kukutana na menejimenti ya halmashauri ya Mji wa Kibaha na kukagua kiwanja ambacho Halmashauri hiyo imekitenga kwa ajili ya MSD kujenga kiwanda cha kuzalishia dawa. Kiwanja hicho ambacho kina ekari 100 kimetengwa katika eneo la Vigwaza - Zegereni Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani. MSD ipo katika hatua za mwisho za mchakato wa kumilikishwa Kiwanja hicho.