MSD yaaswa kuboresha upatikanaji wa dawa
MSD waaswa kuboresha upatikanaji dawa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amewaasa watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD)
kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa. Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo alipokuwa akizindua Baraza la tatu
la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pia amesisitiza kuwa Baraza hilo libuni mbinu na mikakati mbadala za kuboresha utendaji bila kusahau kutii miiko ya utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amemweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa tayari MSD
imeanza kununua dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji, ambapo hadi sasa wana wazalishaji 20 ambao wana mikataba, na wazabuni wengine 76 wa dawa na 79 wa vifaa tiba zabuni zao zinaandaliwa.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makao Makuu ya MSD na Kanda zote nane za MSD ambao ni pamoja na wenyeviti wa TUGHE wa matawi pamoja wawakilishi wa wafanyakazi.