Baraza la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa limefanya uchaguzi
Hii leo tarehe 7/12/2016 Baraza la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa limefanya uchaguzi kwa ajili ya kupata Katibu wa Baraza hilo pamoja na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo.
Wajumbe hao wamepiga kura na kumchagua Christmas Gowele kuwa Katibu na Dominica Meena kuwa Katibu Msaidizi.
Viongozi hao kwa pamoja wameomba ushirikiano kutoka kwa wajumbe wa baraza, ili Baraza hilo liwe la kasi zaidi katika kushirikisha wafanyakazi katika chombo hicho cha ushauri na majadiliano sehemu za kazi.
Kabla ya uchaguzi huo, wajumbe wa baraza walipata fursa ya kupata mafunzo yenye mada mbili, ambazo ni pamoja na Maadili na uadilifu katika utumishi wa umma na dhana ya Baraza la wafanyakazi na wajibu wa wajumbe
wa Baraza la wafanyakazi. Mafunzo hayo yalikuwa maalumu kabisa kwa wajumbe hao, ambao ni wapya katika Baraza hilo jipya la wafanyakazila MSD. Kwa kawaida wajumbe wa Baraza hilo hudumu kwa miaka mitatu kabla ya wajumbe wengine kuteuliwa.