MSD yazindua huduma maalumu kwa wateja wakubwa


Bohari ya dawa (MSD) hii leo tarehe 6/12 /2016 imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma kwa haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitahi mahitaji yao.

Wateja hao ni pamoja na hosipitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, hosipitali ya Kibong’oto, Mirembe, hosipitali za Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.

Dkt. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ili kuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia utasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema, hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo watarajie maboresho makubwa ya huduma.

 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker