Waziri afafanua upatikanaji wa dawa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewahakikishia wananchi kuwa dawa muhimu za kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu zinapatikana Bohari ya Dawa MSD na tayari nyingine zimeshasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Amezitaja dawa hizo kuwa ni pamoja vidonge vya maumivu vya Paracetamol na paracetamol za watoto, dawa ya vidonge na sindano ya Diclofenac, Dawa za kutibu maambukizi (antibiotics) ambazo ni pamoja na Amoxicillin, Co- trimoxazole, Ceftriaxone, Erythromycin na Metronidazole.
Hata hivyo Mheshimiwa Ummy Mwalimu amekiri kuwa tatizo la chanjo lilikuwepo lakini amesema kwa sasa chanjo za Surua, Pepopunda, Homa ya manjano, Kupooza na Kifua Kikuu zipo za kutosha miezi mitatu kuanzia sasa na nyingine zimeshaagizwa.