Watumishi wa MSD wapewa mafunzo ya zima moto

Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, mkoa wa Temeke jijini Dar Es Salaam limetoa mafunzo ya zima moto na uokoaji kwa Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Makao Makuu ambapo pia wamepata elimu ya jumla juu ya uokoaji na kuzima moto kwa vitendo.

Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, mkoa wa Temeke Castory Willa ameeleza kuwa mara nyingi wananchi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu kujiokoa pindi wanapopata matatizo ya moto, hivyo ni vyema elimu kama hizi zikazingatiwa na kufanyiwa majaribio mara kwa mara kwa jamii mbalimbali.

Ameongeza kuwa, cha muhimu ni kujua namna ya kujikinga kwanza, kasha kupiga namba maalumu ya huduma ya zima moto ambayo ni 114 mahali popote mtu alipo nchini.Hata hivyo alieleza kuwa ni muhimu kusaini kitabu cha mahudhurio kazini wakati wa kuingia na kutoka kwani ndicho kitu cha kwanza kufuatilia pindi janga linapotokea kwa ajili ya kuokoa watu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bi. Neema Mwale amesema zoezi hili kisheria linatakiwa kufanyika mara mbili kwa mwaka ili kuhakikisha elimu hii inaeleweka kwa wafanyakazi wote.Mafunzo hayo yalitoa pia fursa ya maswali na majibu, ambapo wafanyakazi walipata fursa ya kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa yanayohusiana na majanga, hasa ya moto.

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker