Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa, lililopo ndani ya hospitali ya Wilaya hiyo na kuzusema kuwa hiyo ni hatua ya serikali ya kuboresha huduma ya afya kwa kuwawezesha wananchi kupata dawa kwa wakati na kwa bei nafuu.

Amesema duka hilo limewekwa wilayani Ruangwa kwasabu eneo hilo lipo katikati ya wilaya za Liwale, Kilwa na Nachingwea hivyo wananchi wa maeneo hayo na hata mikoa jirani watafaidika na huduma hiyo.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka huu wa fedha, serikali imeongeza bajeti ya dawa mara tano zaidi kutoka shilingi Bilioni 29.25 ya mwaka jana hadi Bilioni 251 mwaka huu wa fedha ili kuiwezesha Bohari ya Dawa kujiendesha kwa uhakika zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema MSD sasa ipo katika mchakato wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, ili kuepuka gharama za uagizaji dawa nje ya nchi na uchelewaji wa dawa.

Duka la Ruangwa linafanya maduka ya MSD mpaka sasa kufikia Sita, ikiwa ni pamoja na mengine yaliyopo Arusha, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na Chato.

Naye Mfamasia Mkuu wa serikali amesema, hivi sasa wana utaratibu mpya wa kuzipa hadhi hospitali na vituo vya afya kwa kuangalia uwezo wake na ubora wa utoaji huduma, ili kuweza kuzipa madaraja.

 

 

 

 

 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker