Mkurugenzi Mkuu wa MSD atoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa-keko kwenda Muhimbili

Hivi karibuni vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini vimeripoti taarifa kuhusu dawa za shilingi 2,000,000,000/= (Bilioni Mbili) kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa Keko kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu mwaka 2012.Tunapenda kutoa taarifa kuwa, hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali bungeni kuhusiana na hesabu za Hospitali ya Taifa Muhimbili, ilionyesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu Mei 2012, licha ya kuonekana kwenye Ankara 23 za Bohari ya Dawa. Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa Ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili.

 

 

Baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali (Delivery Notes) za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo. Mali zote hizi zilishapelekwa Muhimbili.

Pamoja na juhudi hizi Bohari ya Dawa imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye Ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba viliyopelekwa hospitalini hapo, kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini Ankara ya kupelekea mali (Delivery Notes) ambazo zote zipo Bohari ya Dawa.

Aidha, mitandao ya kijamii nchini imekuwa inasambaza picha za gari aina ya lori lenye herufi tatu za "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la Bohari ya Dawa lililokwama kwenye daraja.Tunapenda kuwafahamisha wananchi kuwa picha hizo za gari zinazosambazwa siyo mali ya Bohari ya Dawa na nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker