Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (mb), amezindua duka la dawa na maghala matatu ya kuhifadhia dawa ya MSD mkoani Mbeya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (mb), amezindua duka la dawa la MSD mkoani Mbeya na maghala matatu ya kisasa ya kuhifadhia dawa yaliyopo mkoani Mbeya, Tanga na Tabora.

Mhe. Waziri, ameipongeza MSD kwa kupata maghala matatu ya kisasa pamoja na uanzishwaji wa duka la Mbeya ambalo litasaidia upatikanaji wa dawa kwa wananchi wa Mbeya na mikoa ya karibu. Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD vibao viwili vya uzinduzi vinavyowakilisha uzinduzi wa maghala ya Tanga na Tabora.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema ghala na duka lililofunguliwa litaiwezesha MSD kupanua uwezo wake wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba na pia kuongeza uwezo wa kusogeza huduma karibu na wanachi.

Hata hivyo, Bwanakunu ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa msaada wa kiwanja cha hekari tano alioutoa kwa MSD. Kiwanja hicho kipo eneo la Luguruni na ambacho kitatumika kujengea ghala la kisasa la kuhifadhia dawa na vifaa tiba kwa Kanda ya Dar-es-salaam.

Pia amemhakikishia Mhe. Rais kwamba, pamoja na msaada huu wa kiwanja na kwakuwa MSD inamahusiano mazuri na wadau wake wa maendeleo, kwasasa ipo kwenye mazungumzo ili ujenzi wa ghala la Dar-es-salaam uanze mapema iwezekanavyo na ikiwezekana mwezi Julai 2016. Kukamilika kwa ujezi huo utapunguza kiasi kikubwa cha fedha kinacholipwa kila mwaka kama kodi ya pango.

 

 

 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker