Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi amemkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi amemkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bwana Laurean Bwanakunu,kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Msd kanda ya Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi kutoa hati hiyo ya Kiwanja hicho kilichopo eneo la Luguru,wilayani Kinondoni ni itekelezaji wa agizo la Rais,baada ya msd kuonyesha uhitaji wa eneo hilo ili kuondokana na gharama ya kukodisha maghala na majengo ya ofisi kwa Kanda ya Dar Es Salaam.

Akitoa shukrani kwa Serikali,Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema kuwa hatua wanatarajia kuanza ujenzi kwenye kiwanja hicho mwaka ujao wa fedha, ambapo kwa sasa msd inalipa kodi ya shilingi Bilioni Tatu kwa mwaka kwa maghala ya kukodi ya Ubungo,na mwakani wanatakiwa kulipa shilingi Bilioni nne.

 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker