MSD yafungua duka kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, la kuitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufungua maduka kwenye maeneo ya hospitali na vituo vya afya nchini, MSD imetekeleza agizo hilo kwa kuzindua duka la kuuza dawa na vifaa tiba liliopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bwana Donan Mbando.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bwana Donald Mbando akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka

 Mpango wa kuanzisha maduka ya MSD ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka sita wa MSD unaoanzia 2014 hadi 2020 kwa ajili ya kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa urahisi nchi nzima hadi ngazi ya vituo vya afya.

Msimamizi wa duka Betia Kaema akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bwana Donald Mbando na wageni waliofika katika uzinduzi wa duka.Bwana Mbando amesema; hatua hii ya kufungua maduka ndani au karibu na hospitali za rufaa na mikoa ni kwaajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema; Duka la Muhimbili ni la pili baada ya duka la mkoani Mbeya na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba tayari MSD itakuwa na duka kwenye hospitali Seketule mkoani Mwanza na Mount Meru Arusha.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Pof. Idris Mtulia amesema; maduka haya yatawasaidia wananchi katika kupata huduma ya dawa pindi zinapohitajika na kwa gharama nafuu.

 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker