Bohari ya Dawa yakamilisha kupeleka vifaa vilivyonunuliwa na bunge kwa ajili ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI)

Bohari ya Dawa (MSD) hii leo tarehe 23/11/2015 imekamilisha zoezi la kupeleka vifaa tiba kwaajili ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.

BOHARI YA DAWA YAKAMILISHA KUPELEKA VIFAA VILIVYONUNULIWA NA BUNGE KWAAJILI YA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI (MOI)

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amekabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambapo Katibu Mkuu Kiongozi alivikagua na baadae kufanya mkutano na Waandishi wa Habari.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 251 (251,000,000) ni pamoja na vitanda 300,magodoro 300,viti maalumu vya wagonjwa (Wheel chairs) 30, vitanda maalumu vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, shuka 1,695 na mablanketi 400.

 

Bwanakunu ameeleza kuwa ofisi yake ilianza kupeleka vifaa hivyo wiki iliyopita, baada ya maombi hayo kuletwa. Amesema MSD kama mnunuzi, mhifadhi na msambazaji wa dawa na vifaa tiba kwa hospitali, vituo vya Afya na zahanati zote za serikali nchini, imefanya moja ya jukumu lake la kuwauzia vifaa hivyo ofisi ya bunge na kuvisambaza kwa kuvifikisha MOI.

Kwa upande mwingine MSD imegomboa vipuri kwa ajili ya ukarabati wa mashine ya CT Scan na MRI za Muhimbili zilizokuwa zimeharibika, pamoja na mashine moja ya Utra Sound na mashine ya kupigia picha X-ray (Digital X-ray machine) moja. Vifaa vyote hivi vimefikishwa leo Muhimbili.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker