Bohari ya Dawa (MSD) yapeleka vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 251 kwenye Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI)

Bohari ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli.

MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE GHARAMA YA SHILINGI Mil. 251

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa {MSD}, Bwana Laurean Bwanakunu amesema vifaa hivyo vyenye gharama ya shillingi Mil.251 (251,000,000) ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.

MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI siku ya ijumaa ya tarehe 20/11/2015 na kuendelea leo siku ya Jumamosi hadi zoezi hilo litakapokamilika wiki ijayo.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker