Production

 

 

     I.       HISTORIA .

Hapo mwanzao MSD ilijulikana kama Bohari kuu ya dawa (Central Medical Store – CMS). Ilifanya kazi ikiwa chini ya wizara ya Afya lakini ikiwajibika kwa wizara tatu za Afya, Fedha na Ujenzi.  Mara baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika kwa wakati huo alifanya ziara katika mataifa mbalimbali hasa yaliyokuwa ya kijamaa kama China, Urusi, Korea n.k. Moja ya makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Tanganyika na China ilikuwa ni Uchina kuisaidia Tanganyika kujitegemea katika viwanda.  Mwaka 1968 kiwanda cha kwanza cha dawa cha serikali kilifunguliwa maeneo ya Keko jijini Dar es Salaam kwa msaada wananchi ya Uchina. Kiwanda hicho kilifanya kazi kikiwa kinatoa dawa kwa ajili ya kusambazwa nchini kupitia Bohari kuu ya dawa ya wakati huo ambayo sasa ni MSD.

Hata hivyo kulingana na mabadiliko ya uchumi ya kidunia; uzoefu mdogo wa kuendesha viwanda, pamoja na masharti ya shirika la fedha duniani yaani International Monetary Fund (IMF)  na Benki ya Dunia yaani World Bank, kiwanda hicho kililazimika kusitisha uzalishaji miaka ya 1990 na hivyo kubinafsishwa rasmi mwaka 1997 na kuwa na umiliki wa hisa nyingi kwa mwndeshaji binafsi. Mwaka 1993, Bohari ya dawa iliundwa upya kwa Sheria ya Bunge ya mwaka 1993. Sheria hiyo ilitambua Bohari kama taasisi inayojitegemea ikijiendesha kwa kanuni za kibiashara na pia iliibadilisha jina na kuwa Medical Stores Department – MSD na kutambua majukumu matatu ya kununua, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba nchini.

 

II.         WAZO LA KUANZISHA

Wazo la kuwa na viwanda vya dawa lilianza tena kujitokeza mwaka 2013 na 2014 kutokana na ufinyu wa bajeti ya dawa na vifaa tiba nchini, huku msukumo ukiwa ni kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Hatahivyo pamoja na jitihada zilizofanywa kwa wakati huo, ilikuwa vigumu kupata kibali ya kukamilisha ndoto hiyo kutokana na ukweli kwamba Sheria iliyoianzisha MSD haikuruhusu kufanya uzalishaji wa dawa.

 

 

III.         MSD KUONGEZEWA MAJUKUMU.

Mnamo mwaka 2020 wazo la viwanda lilipata msukumo mpya na hatimaye sheria ya MSD ya mwaka 1993 ilifanyiwa marekebisho na pamoja na mambo mengine, liliongezwa jukumu la kuzalisha dawa na vifaa tiba na hivyo kufanya majukumu ya MSD kuwa manne yaani Kununua, kuzalisha, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba nchini. Hivi sasa MSD imeanza kutekeleza jukumu la kuzalisha bidhaa za afya nchini, kupitia viwanda vyake, huku pia ikipeleka msukumo mkubwa kwenye uzalishaji kupitia ubia (PPP) baina yake na kampuni au taasisi mbalimbali zenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya viwanda vya bidhaa za afya nchini.

 

 

IV.         SABABU ZA KUANZISHA VIWANDA VYA MSD.

 

Zifuatazo ni sababu zilizoleta ari ya kuanzisha viwanda vya dawa MSD na Taifa kwa

     ujumla

 

a.    Kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini kwa kupunguza muda wa kuagiza dawa nchi za nje yaaani lead time

 

b.    Kupunguza ununuzi wa bidhaa tiba kwa kutumia pesa za kigeni ambazo nchi inazitafuta kwa jasho.

 

c.     Kuondoa gharama zitokanazo na uagizaji dawa nchi za ng’ambo na kuwa na dawa za bei nafuu lakini zenye ubora wa viwango vya kimataifa.

 

d.    Kutoa ajira kwa watanzania na hivyo kuchangia katika uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

 

e.    Kuwa na usalama wa kitaifa katika bidhaa muhimu za Afya hata wakati wa majanga makubwa ya dunia ambapo uagizaji dawa unakuwa hauwezekani tena.

 

f.      Kuendana na sera ya nchi ya Tanzania ya viwanda

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker