Waziri wa Afya afanya ziara MSD

Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.

Mbali na hilo, waziri huyo wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.

Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.

Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya Makao Makuu, jingo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.

Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.

 

MSD yafungua duka kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, la kuitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufungua maduka kwenye maeneo ya hospitali na vituo vya afya nchini, MSD imetekeleza agizo hilo kwa kuzindua duka la kuuza dawa na vifaa tiba liliopo ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bwana Donan Mbando.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bwana Donald Mbando akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka

Bohari ya Dawa yakamilisha kupeleka vifaa vilivyonunuliwa na bunge kwa ajili ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI)

Bohari ya Dawa (MSD) hii leo tarehe 23/11/2015 imekamilisha zoezi la kupeleka vifaa tiba kwaajili ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.

BOHARI YA DAWA YAKAMILISHA KUPELEKA VIFAA VILIVYONUNULIWA NA BUNGE KWAAJILI YA TAASISI YA MIFUPA YA MUHIMBILI (MOI)

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amekabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambapo Katibu Mkuu Kiongozi alivikagua na baadae kufanya mkutano na Waandishi wa Habari.

Bohari ya Dawa (MSD) yapeleka vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 251 kwenye Taasisi ya Mifupa, Muhimbili (MOI)

Bohari ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli.

MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE GHARAMA YA SHILINGI Mil. 251

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa {MSD}, Bwana Laurean Bwanakunu amesema vifaa hivyo vyenye gharama ya shillingi Mil.251 (251,000,000) ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.

MSD yaihudumia hospitali mpya UDOM

Bohari ya Dawa MSD kanda ya Kati, imepeleka dawa na vifaa tiba kwaajili ya Kituo cha Uchunguzi cha Kimataifa cha UDOM UItra Modern Health Institute, kwaajili ya kituo hicho kuanza rasmi huduma baada ya uzinduzi.

Meneja wa MSD Kanda ya Kati Bwana John Sipendi amesema kuwa baada ya kupata maelekezo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuhusu vifaa tiba na dawa vinavyohitajika walifanya maandalizi na kuvifikisha kituoni hapo mwanzoni mwa wiki hii.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker