Bohari ya Dawa (MSD), imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara

Bohari ya Dawa (MSD), leo imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara jijini Dar es salaam, wenye lengo la kujadili kwa pamoja juu ya changamoto, maboresho, taratibu na sheria mbalimbali za manunuzi zinazotumika hapa nchini, sambamba na kuwashawishi wazalishaji hao kuja kuwekeza nchini kupitia viwanda vya dawa.Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema MSD imejiimarisha na kujijengea uwezo wa kuwahudumia wateja wake, hivyo inapaswa kuwa na uhakika na upatikanaji wa dawa zenye viwango na ubora unaokubalika.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole Gabriel amewahamasisha wazalishaji hao kuchangamkia fursa adhimu ya kuanzisha viwanda vya dawa hapa nchini, kwa kuwa mahitaji ya viwanda vya dawa ni makubwa na kuongeza kuwa, uwepo wa viwanda hivyo utarahisisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema mkutano huo ni hatua muhimu ya kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa pande zote mbili wakati wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha na kurahisisha mazingira ya kibiashara. Mkutano huo ulioenda pamoja na majadiliano umefanyika ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara kati ya wadau hao na MSD, ili kuleta tija katika uzalishaji na upatikanaji wa dawa nchini.

Jumla ya wazalishaji 130 kutoka zaidi ya nchi 25 wameshiriki mkutano huo ikiwa ni pamoja na wadau wengine wa MSD.

Watendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) na watendaji wa Central Medical Store(CMS) wamekutana kwenye kikao kazi

Watendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) na watendaji wa Central Medical Store(CMS) wamekutana kwenye kikao kazi cha kuimarisha mfumo wa mnyororo wa ugavi. Kikao hiki ni muendelezo wa vikao vya  kuwashirikisha wadau hao wa MSD kutoka Zanzibar juu ya mwongozo mpya wa kukadiria matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ulioandaliwa na wataalamu kutoka Wizara ya Afya,GHSC na MSD. Mwongozo huo utaanza kufanya kazi kwenye kukadiria matumizi ya dawa ya mwaka 2019/2020.
 

Watumishi wa Bohari ya Dawa(MSD) wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)

Watumishi wa Bohari ya Dawa(MSD) wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi),ambayo kitaifa mwaka huu yamefanyika mkoani Iringa.
Kanda zote za MSD nchini pia zimeshiriki maadhimisho hayo kwa ngazi ya mkoa na kuwatambua watumishi bora kwa mwaka 2017/2018.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema "Kuunganishwa kwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi "
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Joseph Pombe Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa MSD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Joseph Pombe Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa MSD kwa utendaji wao mzuri na kuwaagiza kushirikiana na wadau wao wengine kuhakikisha wanatatua cha ngamoto za upatikanaji wa viwanda vya dawa nchini.
 
Rais ameyasema hayo alipokuwa kwenye ghafla ya uzinduzi wa magari mapya 181 ya MSD ya kusambazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara,yaliyotolewa msaada na Mfuko wa pamoja wa Kudhibiti UKIMWI, Kujua Mkuu na Malaria (Global Fund). Amewaagiza usimamizi wa magari hayo mapya unzingatiwa na kuangalia madereva wanaofaa wakati wa zoezi la mwajiri.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Rugambwa  Bwanakunu amemshukuru Rais kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka shilingi Bilioni 30(2015/16) na kufikia Bilioni 269(2017/2018) ambayo imewezesha MSD kuondoka na kero ya kulalamikiwa na wateja kutoka na uhaba wa dawa kwenye vituo cha kutolea huduma.
 
Magari hayo 181 yanaongeza idadi ya magari yote ya MSD kuwa 213,baada ya kutoa magari chakavu.Amesema kupitia magari haya mfumo  wa usambazaji dawa wa moja kwa moja hadi kwa wateja ngazi ya kijiji utabadilika kutoka mara nne kwa mwaka kuwa mara sita kwa mwaka.

MSD yatunukiwa ithibati ya juu ya ubora ISO 9001:2015

Bohari ya dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi,utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).

Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uliofanywa na kampuni ya  Kimataifa ya ACM LIMITED mwezi Agosti 2017, na kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozo ya  ya juu ya kimataifa katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na kuboresha masuala yote yanayohusiana na mnyororo wa ugavi wa ili kuwapa wananchi huduma bora, zenye viwango, bei kwa nafuu na kuwafikishia kwa wakati.

Bwanakunu ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa ugavi wa MSD kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wa mwaka 2017 - 2020.

Mara ya kwanza MSD ilipata Ithibati ya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza kuishikilia   ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa.

   

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker