Bohari ya Dawa (MSD) yazindua mpango wa kukusanya shilingi bilioni 21 kwa mwezi

Bohari ya dawa (MSD) imezindua mpango wa kukusanya shilingi Bilioni 21 kutoka kwenye makusanyo ya mauzo ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa mwezi Julai mwaka 2017. Utaratibu huo utakuwa unawekwa kila mwezi kama katika mwaka huu wa fedha.

Mpango huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu kulingana na maelekezo ya Serikali kuwa tunatakiwa kukusanya wastani wa shilingi Bilioni 21kila mwezi.

Mpango huu unaendana na dhana ya kuboresha huduma kwa wateja, kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati wote, kuhakikisha Kanda zote zina mahitaji wanayoomba, kuhakikisha .

Akizindua mpango huu Kaimu Mkurugenzi Mkuu Victoria Elangwa amesema kuanzia mwezi huu wa Julai, wameamua na kudhamiria kuanza kufikia kiwango hicho cha mauzo cha shilingi Bilioni 21, hivyo wafanyakazi wajitume na kuhakikisha wanaboresha huduma zaidi kwani kama tuliweza kufikia makusanyo ya shilingi Bilioni 16 mwezi MEI, mwaka huu, basi hata hili tulichukue kama jambo linalowezekana.

Kanda ya Dar es Salaam (MSD) yaanza kutoa huduma

Baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu mali la kufunga mwaka wa Fedha wa 2016/2017, huduma kwa wateja kwenye Kanda zote 8 za MSD pamoja na vituo vya

mauzo viwili zimerejea kama kawaida, huku wafanyakazi wakiwa wameanza kuhudumia maombi mbalimbali ya dawa yaliyowafikia kutoka kwa wateja.

Mameneja wa Kanda za Mbeya, Benjamin Hubila pamoja na Kanda ya DSM Celistin Haule wamesema wameanza kuwahudumia wateja wao kwa mahitaji waliyoanza

kuleta ikiwa ni baada ya zoezi la kuhesabu mali ambalo lilifanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 15 Juni, 2017 na kukamilika tarehe 30 Juni, 2017.

Mwenyekiti wa Zoezi la kuhesabu mali kwa mwaka huu Meritus Magungu amesema zoezi la kuhesabu mali mwaka huu limeenda vizuri kwa siku zilizopangwa, hasa

kwa kuzingatia matumizi ya msimbo mpao (Barcord) ambao umesaidia kupata taarifa sahihi kwa muda mfupi. Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa asilimia 99.9.

Aidha ameongeza kuwamatumizi ya Barcord yameweza kupunguza tofauti za taarifa zilizopo kwenye mitandao na za mali halisia (discrepancy).

 
--

MSD yakutana na washitiri na wazalishaji

Bohari ya dawa (MSD) imefanya mkutano na washitiri, watoa huduma na wazalishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara wanaotoka ndani na nje ya nchi kujadili kuhusu maboresho ya manunuzi ya bidhaa za MSD.

Takribani wazalishaji hao wanatoka nchi za Kenya, Uganda, India, Bangladesh, China, Korea, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika Kusini.

Tangazo la Kuhesabu Mali

Bohari ya Dawa (MSD) inawaarifu wateja wake wote wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuwa; kuanzia tarehe 15/6/2017 mpaka tarehe 30/6/2017 litafanyika zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria. Kutokana na zoezi hilo la kuhesabu mali, maghala yote ya MSD  yatafungwa kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia tarehe 15/6/2017.

Maombi yote ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara yawasilishwe MSD kabla ya tarehe 7/6/2017, ili kukidhi mahitaji wakati wote maghala yetu yatakapokuwa yamefungwa. 

Aidha, huduma ya dharura ya kupata mahitaji itatolewa, pale tu itakapothibitika uhitaji.

MSD yakarabati Ghala la dawa la Mirembe


Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na ukarabati huo,watoa ushieikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa yenye utaalamu unaohitajika.Ameongeza kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo,ikiwa ni pamoja na kukopeshwa,kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na kuomba ushirikiano zaidi na MSD,ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker