MSD Yashinda Tuzo 3 za Mwajiri Bora

ate.jpg

 

 

Bohari ya Dawa (MSD) imeshinda tuzo 3 za Mwajiri bora za ATE kwa mwaka (2018) na kwa mara ya kwanza imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumi bora kwa mwajiri bora Tanzania.

 

atee.jpg

MSD ni kati ya waajiri 59 waliofikia hatua ya mchujo huo na tuzo walizoshinda MSD ni pamoja na Mwajiri Bora anayeangalia USTAWI wa wafanyakazi (employee WELLNESS), Mwajiri Bora wa kizalendo (Overall best local winner) na Mwajiri Bora katika utumishi wa Umma.

ateee.jpg

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi.Victoria Elangwa amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano madhubuti kati ya wafanyakazi menejimenti na Wizara, utekelezaji mzuri wa mpango mkakati wa MSD pamoja na mahusiano bora na chama cha wafanyakazi.

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amefurahishwa na tuzo hizo na kuwapa rai wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili wapate tija zaidi kama kauli mbiu ya taasisi inavyosema; "Tumedhamiria kuokoa maisha yako".

ateeeee.jpg

 

Tuzo hizo zilitolewa jijini DSM na Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama.

MSD na Aga Khan,Tanzania Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano.

aghakhan_5.jpg

 

Bohari ya Dawa (MSD) na Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan,Tanzania(AKHST) wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano ambapo MSD itaiuzia hospitali ya Aga Khan dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

 

 

Makubaliano hayo pia yatahusisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye maeneo ya mafunzo, kubadilishana uzoefu kwa taasisi hizo mbili kwenye mitandao ya mnunuzi,kwani MSD ina wazalishaji zaidi ya 130 huku Aga Khan ikiwa mitandao ya kimataifa. Hatua hii itafanya ununuzi wa dawa maalumu na za hospitali za Rufaa kuwa rahisi na kwa bei nafuu.

 

 

 

Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Huduma za Afya Aga Khan, Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Sulaiman Shahabuddin, MSD Dar es Salaam.

 

 

MSD Yapata Bodi Mpya ya Wadhamini

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) ambayo mwenyekiti wake ni Dr.Fatma Mrisho.

 

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni pamoja na Bi. Uphoo Swai, Dkt. Eliamini Sedoyeke, Bw. Ahmed Shaaban Kilima, Bw. Mwemezi Elnathan Ngemera, Bw. Lubengo Hilary Nyang’ula, Prof. Eligius Francis Lyamuya na Dkt. Marina Daula Njelekela huku mjumbe mwingine wa Bodi hiyo akitegemewa kuteuliwa hivi karibuni.

 

Mhe. Ummy amewataka wajumbe wa bodi hiyo, kufanya kazi kama timu moja kwa kutumia taaluma na weledi wao ili kuhakikisha wanasimamia vyema utendaji wa shughuli za Bohari ya Dawa na kufikia viwango bora vya ufanisi zaidi katika ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

 

Aidha amewasihi wajumbe hao kuhakikisha MSD inajiendesha kibiashara, sambamba na kuzingatia taratibu za kitaalamu zinazohusiana na usimamizi na udhibiti wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na maelekezo ya sheria ya manunuzi ya umma.

 

Waziri Ummy ameielekeza bodi hiyo kuhakikisha Bohari ya Dawa inajiendesha vyema kifedha na shughuli zake kuendeshwa kwa gharama nafuu, kuziba mianya yote ya rushwa, wizi na ubadhirifu wa aina yoyote ile, upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vyenye ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa na mwisho kusimamia, kuboresha na kudumisha matumizi ya tehama ili kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu ya Bohari ya Dawa.

MSD na Sekretarieti ya SADC Wasaini Makubaliano ya Ununuzi wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa Ajili ya Nchi za Jumuiya ya SADC.

SADC2.jpg

Katibu Mtendaji wa Sekretariet ya SADC Dkt. Stergomena L. Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu wamesaini mkataba wa makubaliano ya MSD kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC).

 

Hatua hii inafuatia uteuzi wa serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ulifanywa wakati wa mkutano wa SADC wa mawaziri wa Afya wa nchi wanachama, uliofanyika mwezi Novemba, 2017 nchini Afrika Kusini.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema tangu wakati huo hadi sasa wamekuwa wakishirikiana na na Sekretarieti ya (SADC) kuandaa rasimu ya mpango wa utekelezaji wa manunuzi ya pamoja yaani SADC Pooled Procurement Services (SPPS).

 

Amesema kulingana na mpango huo, uratibu wa manunuzi unaanza rasmi tarehe leo, tarehe 9/10/2018, kupitia mkataba wa makubaliano yaani Memorandum of Understanding (MoU) kati ya MSD na Sekretarieti ya SADC.

Bwanakunu ameongeza kuwa MSD itakuwa na majukumu ya kupokea mahitaji ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa nchi hizo 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),  kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, kusimamia takwimu na taarifa za dawa pamoja na kusimamia Kanzidata (Database) ya dawa za nchi hizo.