Mwenyekiti wa Bodi MSD, Aipongenza Menejimenti ya MSD na Wafanyakazi

BARAZA_3.jpg

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho ameipongeza Menejimenti ya Bohari ya Dawa(MSD) kwa kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa wateja wake pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri na wadau wake mbalimbali.

 

BAZARA_6.jpg

Dkt.Mrisho amesema hayo alipokuwa akifungua  kikao cha 17 cha Baraza la wafanyakazi la MSD,kinachoendelea mjini  Dodoma.

 

Mwenyekiti huyo amewataka watumishi  wa MSD kuhakikisha wanafanya kazi kwa umakini kwa kuzingatia dhamira na nia ya kuundwa kwa MSD inafanikiwa,kwa kuhakikisha dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vyenye ubora vinapatikana  nchi nzima na kwa nchi za Ukanda wa SADC kwa wakati na kwa bei nafuu.

 

BARAZA5.jpg

 

 

 

MSD Yashinda Tuzo 3 za Mwajiri Bora

ate.jpg

 

 

Bohari ya Dawa (MSD) imeshinda tuzo 3 za Mwajiri bora za ATE kwa mwaka (2018) na kwa mara ya kwanza imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumi bora kwa mwajiri bora Tanzania.

 

atee.jpg

MSD ni kati ya waajiri 59 waliofikia hatua ya mchujo huo na tuzo walizoshinda MSD ni pamoja na Mwajiri Bora anayeangalia USTAWI wa wafanyakazi (employee WELLNESS), Mwajiri Bora wa kizalendo (Overall best local winner) na Mwajiri Bora katika utumishi wa Umma.

ateee.jpg

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi.Victoria Elangwa amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano madhubuti kati ya wafanyakazi menejimenti na Wizara, utekelezaji mzuri wa mpango mkakati wa MSD pamoja na mahusiano bora na chama cha wafanyakazi.

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amefurahishwa na tuzo hizo na kuwapa rai wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili wapate tija zaidi kama kauli mbiu ya taasisi inavyosema; "Tumedhamiria kuokoa maisha yako".

ateeeee.jpg

 

Tuzo hizo zilitolewa jijini DSM na Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama.

MSD na Aga Khan,Tanzania Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano.

aghakhan_5.jpg

 

Bohari ya Dawa (MSD) na Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan,Tanzania(AKHST) wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano ambapo MSD itaiuzia hospitali ya Aga Khan dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

 

 

Makubaliano hayo pia yatahusisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye maeneo ya mafunzo, kubadilishana uzoefu kwa taasisi hizo mbili kwenye mitandao ya mnunuzi,kwani MSD ina wazalishaji zaidi ya 130 huku Aga Khan ikiwa mitandao ya kimataifa. Hatua hii itafanya ununuzi wa dawa maalumu na za hospitali za Rufaa kuwa rahisi na kwa bei nafuu.