Rais Magufuli Aipaisha Sekta ya Afya

 

Patrobass_Katambi-_DC.jpg

                                MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini, Patrobass Katambi, akizungumza na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) na waandishi wa habari jijini Dodoma,

 


MKUU wa Wilaya ya Dodoma mjini,Patrobass Katambi amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameipaisha sekta ya afya maradufu
kwa kutenga bajeti kubwa ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi
vya maabara tangu aingie madarakani.

Katambi aliyasema hayo wakati akizungumza na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) waliopo mkoani Dodoma kutembelea wateja wao
ili kujua changamoto zilizopo ili zitafutiwe ufumbuzi baada ya MSD kufanya maboresho makubwa ya upatikanaji wa dawa nchini.

 

"Kwa kweli Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wamefanya kazi kubwa ya upatikanaji wa dawa, ujenzi wa vituo vya afya vya kisasa na maboresho mbalimbali katika sekta hiyo"
alisema Katambi.

 

Alisema baada ya vituo hivyo vya afya kuboreshwa miundombinu yake na kujengwa vingine vimekuwa kama Hospitali za wilaya za

miaka ya nyuma.Alisema Dodoma hivi sasa kuna Hospitali kubwa mbili ya Benjaminil Mkapa na ya General na zote zinatoa huduma

nzuri bila ya kuwepo malalamiko yoyote.

 

Katambi alisema Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuona Jiji la Dodoma siku za mbeleni kuja kuwa na ongezeko kubwa la watu alitoa

milioni 950 ambazo zilikuwa zitumike katika sherehe ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru ili ijengwe Hospitali kubwa itakayoitwa Uhuru

itakayojengwa Chamwino.

 

Aliongeza kuwa katika Jiji la Dodoma hakuna tena changamoto ya ukosekanaji wa dawa na vifaa tiba na hiyo imetokana na ubunifu, mifumo ya kisasa na mapinduzi makubwa ya kiutendaji yaliyofanywa na MSD.

 

Alisema kazi inayofanywa hivi sasa na MSD ni ya kimataifa kwani wana magari ya kutosha ya usambazaji wa dawa nchi nzima, wafanyakazi wake wapo nadhifu wakati wote na dawa zinawafikia walengwa kwa wakati jambo linalowafanya wananchi kuwa na

imani na MSD.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker